Star Tv

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa NASA Raila Odinga leo March 9, 2018 wamekutana rasmi na kuzungumza.

Viongozi hao wamekutana na kuzungumza kuhusu kuacha tofauti zao za kisiasa na kutanguliza maslahi ya wananchi wa nchi hiyo kwanza kwa kufanya kazi pamoja kurudisha amani.

“Maisha yetu ya baadaye hayawezi kupimwa kwa Uchaguzi Mkuu unaofuata bali utulivu wa nchi yetu na hali nzuri ya watu wetu, demokrasia ni mchakato ambao, hiari ya watu inasikilizwa lakini maslahi ya taifa lazima yatawale.” – Uhuru Kenyatta

Kwa upande wake Raila Odinga ameeleza kuwa “tukiendelea kuwa wabinafsi na waharibifu, hakuna kiwango chochote cha mageuzi ya kitaasisi ambacho kitaboresha maisha yetu.”

Inaelezwa kuwa wawili hao wamekubaliana kushirikiana katika agenda 9 mahususi, na ipo kamati iliyoundwa itakayo husisha wajumbe wa pande zote mbili ili kuanzisha programu ya kuwaunganisha tena wananchi ambao walitengwa na milengo ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.