Rwanda na Kenya zimeanza kutoa chanjo kwa watoto ambapo wamebainisha kuwa sasa watoto nchini mwao wanastahili kupokea chanjo ya Pfizer huku nchi zote mbili zikianzisha kampeni za chanjo kwa rika hilo.
Rwanda itakuwa ikiwachanja watoto wenye umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea kuanzia Jumanne huku Kenya ikiwaruhusu wale wenye umri wa kuanzia miaka 15.
Rwanda ina idadi kubwa zaidi ya watu waliopata chanjo kamili katika Afrika Mashariki ikiwa na zaidi ya 20% ya jumla ya watu wote.
Mpango wa chanjo ya vijana wa Rwanda utashughulikia nchi nzima na wazazi au walezi wanapaswa kutia saini fomu za idhini kabla ya watoto wao kupewa chanjo.
Rwanda imebainisha kuwa itafanya kazi na shule kwa usambazaji na ukusanyaji wa fomu za idhini.
Nchini Kenya, Wizara ya Afya inatarajia kupokea dozi milioni nne za chanjo ya Pfizer kwenye kampeni yake ya kuwachanja vijana.
#ChanzoBBCSwahili