Star Tv

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Kamanda wa vikosi vya ardhi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametoa taarifa ya uzinduzi wa gari hilo kwa kuweka picha katika ukurasa wake Twitter,  picha ya kile anachosema kuwa gari la kwanza la kivita kutengenezwa nchini humo.

Anasema "liliundwa na kutengenezwa ncini Uganda", lakini hakutoa maelezo kuhusu muundo na gharama yake.

Gari hilo lililopewa jina la Chui lilizinduliwa na baba yake ambaye pia ndio Amiri Jeshi mkuu wa Taifa hilo, Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Jeshi la Uganda mwaka jana lilihusika katika msako mkali dhidi ya maandamano yaliyotikisa mji mkuu, Kampala, kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais Bobi Wine.

Maafisa wa Jeshi nchini humo walitetea utumizi wa silaha za moto, wakisema polisi na jeshi walikuwa wakikabiliana na waandamanaji.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.