Star Tv

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima juhudi zozote za kuzua ghasia baada ya kuchaguliwa kwake tena.

Museveni amewaambia wanahabari katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura nje ya mji mkuu Kampala kwamba hakuna atakayezua ghasia katika eneo hilo kwa sababu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakabiliwa vilivyo.

Rais Museveni ameongeza kuwa hakuna mtu anayewashinda katika matumizi ya bunduki na pia mapigano.

David Rubongoya ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Upinzani, National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Bobi Wine ambaye jina lake rasmi ni Robert Kyagulanyi, aliyeshindwa na Museveni katika uchaguzi huo wa rais, ameliambia shirika la habari la dpa kwamba maafisa wa usalama wameanza kuwakamata wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Katika taarifa, jeshi la polisi nchini Uganda limesema kuwa limewakamata takriban watu 84 kuhusiana na ghasia za uchaguzi.

Lakini kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa chama cha NUP Joel Ssenyonyi amesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wakiwatesa kwa utaratibu washirika wa upinzani.

Ssenyonyi amesema kuwa Uganda iko kama katika vita, huku maafisa wa polisi na Jeshi wakipelekwa kila mahali kuwakamata wafuasi wa upinzani.

Makazi ya Wine, msanii aliyegeuka kuwa mwanasiasa yaliyoko kwenye mji mkuu, Kampala yamezingirwa na wanajeshi tangu Ijumaa jioni na kumfanya kuwa chini ya kifungo cha nyumbani.

Mapema jana, tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza Museveni mshindi wa uchaguzi huo wa rais baada ya kupata kura milioni 5.85 huku mpinzani wake wa karibu Wine akipata kura milioni 3.47.

Wakati huo huo, Uingereza imetoa wito wa kuchunguzwa kwa malalamiko ya uchaguzi huo wa urais uliokamilika nchini Uganda ambapo Rais Museveni ametangazwa kuwa mshindi.

Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Afrika James Duddridge, amesema kuwa raia wengi nchini Uganda na nje wameelezea wasiwasi kuhusu mazingira jumla ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi pamoja na mchakato mzima wa uchaguzi.

Duddridge amesema kuwa ni muhimu kwa wasiwasi huo kuelezwa, kuchunguzwa na kutatuliwa wa njia ya amani, kisheria na kikatiba.

Marekani kwa upande wake imeelezea wasiwasi kuhusu taarifa za ghasia na dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo mkuu wa Uganda.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.