Star Tv

Mamlaka nchini Uganda ilikatiza huduma za intaneti saa kadhaa kabla ya uchaguzi wa urais unaokumbwa na ushindani mkali kati ya Bobi Wine na Yoweri Museveni.

Kundi la ufuatiliaji wa masuala ya Itaneti NetBlocks liliandika kwenye Twitter yake kwamba nchi hiyo ilizima mitandao yote ya intaneti Jumatano saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo ilifuatia agizo la serikali kufungia mitandao yote ya kijamii na programu tumishi za kutuma ujumbe.

Rais Yoweri Museveni alisema alifikia uamuzi huo kwa sababu Facebook ilifunga akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.

Mgombea wa urais,mwanamuziki aliyegeuka Bobi Wine aliandika katika Twitter yake kwamba huduma za intaneti zimekatizwa kama sehemu ya njama ya kuiba kura.

"Watu wa Uganda wako imara na hakuna jambo lolote litakatiza azma yao ya kikomesha utawala wa kiimla,"- aliongeza.

Shughuli za upigaji kura ilianza saa moja asubuhi ya leo Alhamisi Januari 14,2021, japo matokeo hayatarajiwi kutolewa kabla ya Jumamosi.

Kampeni za uchaguzi zilikumbwa na ghasia ambazo zilisababisha vifo vya makumi ya watu.

Bw. Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.