Star Tv

Pembe la Afrika bado linakabiliwa na uvamizi wa nzige wa jangwani.

Hii ni kutokana na makundi mapya ya nzige wa jangwani yanayotarajiwa nchini Ethiopia na Somalia katika wiki zijazo. Kisha wataenea hadi Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo (FAO) limeonya.

Pembe la Afrika linatishiwa na uvamizi mbaya wa nzige wa jangwani baada ya ule wa miaka 70 iliyopita. Mabilioni ya nzige ambao walivamia kanda hii mwaka huu, wakiharibu makumi ya maelfu ya hekta za mazao, wamezaliana tena.

Nzige wa kike hutaga mayai zaidi ya mia moja kwa wastani, Hivyo watoto wanaotoka kwenye mayai hayo wanaweza kuongezeka mara 20 kila miezi mitatu. Mabuu, ambayo yamefikia hatua ya kukomaa kwa kuanza kuruka, sasa yanaunda makundi haya mapya.

“Nzige tayari wameonekana nchini Yemen na Kaskazini mashariki mwa Ethiopia. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, watakuwa wamevamia Ethiopia mashariki na Somalia ya kati, Alafu Kaskazini mwa Kenya itakumbwa tena mnamo mwezi Novemba”-Shirika la FAO limebaini.

Wimbi hili jipya linatokana na upepo mkali kutoka Yemen ambao ulienea juu ya Pembe la Afrika, ukibeba mawingu haya makubwa meusi ya mabilioni ya nzige wa jangwani.

Kwa uvamizi wa kipekee wa nzige wa jangani uliorekodiwa mwaka huu tayari umeharibu maelfu ya hekta za mazao na malisho katika Pembe la Afrika, na kusababisha shida kubwa ya chakula.

Joto pamoja na mvua kubwa mwishoni mwa mwaka 2019 hadi Februari 2020 ni chanzo cha hali hiyo, FAO imeonya.

Aidha, Shirika la FAO limeeleza kuwa kuna suluhisho moja tu la kushinda tatizo hilo ambapo ni kwa kunyunyizia dawa wadudu hao.

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.