Star Tv

Chama cha wanasheria nchini Kenya pamoja na makundi kadhaa ya kupigania haki na demokrasia, yamemtaka rais Uhuru Kenyatta hadi kufikia tarehe 12 ya mwezi huu wa Octoba awe amelivunja bunge kwa kuzingatia ushauri wa Jaji Mkuu David Maraga.

Kumekuwa na mjadala ikiwa rais Kenyatta alivunje bunge au kutafuta suluhu nyingine kuhusu suala lililoibua utata wa kikatiba kuhusu theluthi mbili ya wanawake katika uongozi.

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, alimshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Senete, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili.

Katiba ya Kenya inataka sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia bungeni kutotawala katika nyadhifa za uteuzi, na kwa miaka 10 sasa wabunge, ambao wengi ni wakiume, wameshindwa kupitisha sheria hiyo.

Jaji Maraga alilaumu wabunge na maseneta wamekwenda kinyume cha Katiba ya mwaka 2010 iliyowataka kutunga sheria hiyo.

Hata hivyo Spika wa bunge Justin Muturi ameendelea kupingana na hoja hiyo akisema kwamba kuvunjwa kwa bunge ni chaguo lisilowezekana.

Katiba mpya ya Kenya ilizinduliwa 2010, na sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili ilifaa kuidhinishwa baada ya miaka mitano.

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.