Star Tv

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwezi ujao.

Hatua hiyo inakuja wakati Uganda kufikia sasa imerekodi visa 5,380 vya maambukizi ya virusi vya Corona, Ambapo wanafunzi Milioni 1.2 walioko kwenye madarasa ya mwisho ya kufanya mitihani ndio watakaoruhusiwa kurejea tena shuleni, baada ya serikali nchini humo kulegeza zaidi ya masharti ya kupambana na janga la Corona.

Rais Museveni amesema wanafunzi hao watarejea Shuleni kuanzia tarehe 15 Oktoba, na mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Shule zilifungwa nchini humo mwezi Machi baada ya kuzuka kwa janga hilo ambalo limewaambukiza watu 6,287 na wengiene 63 kupoteza maisha.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan,China, na baadaye vilianza kusambaa kwenye mataifa mengine, Ambapo mpaka sasa baadhi ya mataifa yako kwenye katazo la kutokutoka nje huku mengine yakiondoa katazo hilo.

Latest News

AKAMATWA NCHINI AUSTRIA AKIWA AMEIBA VINYONGA 74 KUTOKA TANZANIA.
27 Jan 2021 07:39 - Grace Melleor

Vinyonga 74 wameokolewa na kupelekwa kwenye bustani ya wanyama ya nchini Austria baada ya kubainika wakiwa kwenye sanduk [ ... ]

RAIS JOE BIDEN AMUONYA RAIS WA URUSI VLADMIR PUTIN
27 Jan 2021 06:39 - Grace Melleor

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.