Star Tv

Wakati hekaheka za maandalizi kuelekea michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kwa vikosi 20 vitakavyoshiriki ligi hiyo, Klabu ya Yanga iliyoweka kambi Mkoani Morogoro, imetangaza kuvunja mkataba na aliyekuwa golikipa namba moja wa kikosi hicho Mcameroon Youthe Rostand.

Awali, Viongozi wa klabu hiyo walipanga kumpeleka kwa mkopo klabu yake ya zamani ya African Lyon itakayoshiriki ligi kuu msimu ujao, lakini kabla dili hilo halijakamilika Rostand akaomba kuvunjwa kwa mkataba wake uliosalia mwaka mmoja akieleza kusumbuliwa na matatizo ya kiafya hivyo hatoweza kukitumikia kikosi hicho kikamilifu, taarifa iliyothibitishwa na Afisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten.

Rostand anakuwa mchezaji wa tatu kuondoka klabuni hapo kabla ya msimu kuanza akitanguliwa na mshambuliaji Obrey Chirwa na beki wa kulia Hassan Kesy, huku hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo ikielezwa kuwa taabani kufuatia siku chache zilizopita Kaimu Katibu Mkuu wake Omary Kaaya kutangaza kutembeza bakuli kuomba michango kutoka kwa wanachama na mashabiki ili kukinusuru kikosi hicho kinachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.