Israeli na Bahrain zimefikia makubaliano ya kufufua uhusiano wao Septemba 11,2020, mwezi mmoja baada ya makubaliano kati ya Falme za Kiarabu na nchi hiyo ya Kiyahudi.
Tangazo hilo pia lilitolewa, wakati huo huo, na rais wa Marekani Donald Trump, wakati mkataba huo unatarajiwa kutiwa saini rasmi katika Ikulu ya White House wiki ijayo.
Bahrain na Israeli sawa na nchi nyingine za Kiarabu katika ukanda huo zimeendelea kuwa na uhasama na Iran.
Tangazo la mkataba wa kufufua uhusiano kati ya Israeli na nchi ya Kifalme ya Bahrain lilitolewa wakati mmoja katika Ikulu ya White House na rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
CHANZO:rfi Swashili.