Star Tv

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameondoa masharti ya usafiri wa kuingia na kutoka katika miji ya Nairobi, Mombasa na Mandera kaskazini mwa nchi.

Katika hotuba yake kwa taifa kuhusu mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona rais Kenyatta amesema hatua ya kufungua miji hiyo mitatu ''inawaweka Wakenya'' katika hali hatari na hivyo basi naomba tuwe waangalifu.

Bw. Kenyatta hata hivyo ametangaza kuwa muda wa kutotoka nje usiku kati ya saa saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri umeongezwa kwa siku thalathini.

''Lazima tutambue tuko katika hatari zaidi ya vile tulivyokuwa wakati kuna masharti, tutachunguza mienendo ya watu, na kama hali itakuwa mbaya tena tutarejea katika lockdown'' Alisema Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta pia ametangaza kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu kwa awamu kwa kuzingatia muongozo wa kuzuia maambukizi ya corona uliowekwa na Wizara ya Afya.

''Tusidanganyane kwamba ugonjwa haupo sana, twasikia watu wakisema huu ugonjwa sio wa kweli kwasababu hakuna mtu anayemjua mtu aliyeambukizwa''.alisema rais Kenyatta.

Wakati huo huo Bw. Kenyatta amewasihi viongozi wote wakiwamo wa kidini kuchukuwa jukumu la kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Maeneo ya kuabudu yametakiwa kuwa na waumini wasiozidi 100 katika kila ibada itakayofanyika na ibada zitafanyika si zaidi ya kipindi cha saa moja, ambayo yanatarajiwa kufunguliwa wiki tatu zijazo baada ya kufanya mashauriano baina ya viongozi wa kidini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.