Star Tv

Msemaji wa serikali na pia Waziri wa Habari wa Sudani Kusini Michael Makuei amesema kuwa mawaziri kumi wa serikali ya nchi hiyo wameambukizwa virusi vya corona.

Hii ni siku chache baada ya Makamu wa rais wa Sudani Kusini Riek Machar na mkewe kuthibitishwa kuwa virusi vya Corona.

Mawaziri wote 10 walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na Corona nchini humo.

Tayari mawaziri wote 10 walioambukizwa virusi hivyo wamejitenga na wote wanaendelea vizuri kiafya, kulingana na taarifa iliyotolewa na serikali.

Sudani kusini ina wagonjwa wa Corona 481, watu wanne wamepona na wengine wanne wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Virusi vya corona vinaendelea kusababisha vifo na mdororo wa uchumi duniani kote, huku bara la Afrika likirekodi visa vya 96,829 vya maambukizi, na vifo 3,031 vinavyotokana na ugonjwa huo kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Corona cha Umoja wa Afrika, CDC.

Kufiki sasa ugonjwa wa COVID-19 umeua watu 333,000 duniani kote, huku watu Milioni 5.11wakiwa wameambukizwa virusi hivyo.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.