Star Tv

 

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amewataka wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa Watanzania pamoja na raia wa Kenya kutumia changamoto ya ugonjwa wa Corona katika kuimarisha undugu, urafiki na umoja uliokuwepo tangu enzi na enzi.

Balozi Kazungu amesema kuwa Rais Uhuru Kenyatta haiangalii Tanzania kama jirani, badala yake anaiona nchii hii kama ndugu yao wa karibu.

Amesema Rais huyo wa Kenya katika moyo wake anawachukulia Watanzania kuwa si majirani bali ni ndugu, na hivyo kunapaswa kuwa na uelewano zaidi kwani watu ni walewale wenye umoja, ili kuendelea kufanya biashara, na kupigana na umaskini.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari Balozi Kazungu amesema kuwa:"Tuzidi kupigana na adui mmoja tu kirusi cha Corona, ambacho hakikuzaliwa Dar es Salaam, Mombasa, Malindi ama Nairobi, kimefanya kuja hapa na kisitutatanishe

Hii ni kutokana na siku kadhaa baada ya kuanza matamko ya kufunga mipaka baina ya Kenya na Tanzania ambapo Balozi wa Kenya nchini hapa Dan Kazungu leo amezungumza na waandishi wa habari na kutoa wito wa kuendeleza umoja na mshikamano, na kamwe ugonjwa huu usipunguze undugu uliokuwepo.

 

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.