Star Tv

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 672 baada ya wagonjwa wapya 23 kukutwa na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24.

Katibu Msimamizi wa masuala ya Afya nchini Kenya Dokta Rashid Aman ametoa taarifa ya ongezeko la Wagonjwa hao katika mkutano wake na waandishi wa habari nchini humo leo Jumapili Mei 08.

Katibu huyo ametaja pia idadi ya waliopona virusi kuwa imefikia 239 baada ya wagonjwa wengine 32 kupona leo.

Katika idadi hiyo, Wagonjwa 12 wameripotiwa kutoka Mombasa , 06 kutoka Mandera 04 kutoka Nairobi na mmoja kutoka Kajiado.

Dkt. Aman amesema kwamba wagonjwa watatu walikuwa wakitoka katika vifaa vya karantini.

Aidha amebainisha kuwa sampuli 32,097 tayari zimekwishafanyiwa vipimo nchini humo mpaka kufikia sasa.

Ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo, Serikali nchini humo imewaagiza madereva wote wa malori ya masafa marefu kufanyiwa vipimo vya lazima saa 48 kabla ya kuanza safari zao.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.