Star Tv

Mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ukerewe Marehemu Masoud Mohamed ambaye alijozolea umaarufu mkubwa mitandaoni baada ya video zake kusambaa akisoma Quran Tukufu yamefanyika leo alasiri mkoani Tabora.

Mazishi ya Marehemu Masoud mbali na kuhudhuriwa na ndugu, wafanyakazi wenzake na majirani pia baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Dini walihudhuria mazishi hayo akiwemo mwakilishi wa Mufti Mkuu nchini.

Marehemu Masoud ni mmoja wa Maaskari waliobadilishwa vituo vya kufanyia kazi hivi karibuni akitokea kituo cha kazi cha Bunda Mkoani Mara.

Marehemu alikutwa na umauti Mei 08, akiwa hotelini mahali alipofikia wakati ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi Wilayani Ukerewe ambapo alikuwa akiishi baada yakukosa nyumba na hivyo alikuwa akitekeleza majukumu yake wakati anasubiri kutafutiwa nyumba ya kuishi.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.