Star Tv

Serikali ya China imesema inajiunga na ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya kukabiliana na virusi hatari vya Corona.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi.Hua Chunying amesema kwamba serikali ya Beijing inakaribisha kujiunga na ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa wa WHO kwa ajili ya kuharakishwa utafiti na uzalishaji wa vifaa vya afya vinavyohusiana na virusi vya Corona.

Chunying ameongeza kwamba serikali ya China inaunga mkono nafasi ya Shirika la Afya Duniani katika mapambano yake dhidi ya Corona na hivyo inakaribisha na kushiriki katika ubunifu na mapendekezo ya shirika hilo kwa lengo la kuharakisha shughuli za kufanyika utafiti, uzalishaji na kugawa chanjo na dawa za kukabili virusi vya Corona.

Kabla ya hapo, Tedros Adhanom Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani alitangaza kuzinduliwa kwa ubunifu wa ushirikiano wa kimataifa huku akionyesha matumaini kwamba China itajiunga na mpango huo.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.