Star Tv

Chuo cha Marekani kimethibitisha watu walioambukizwa virusi vya corona kufikia zaidi ya Milioni moja, ambapo idadi hiyo ni sawa na karibu  ya theluthi moja ya idadi yote duniani.

Chuo cha Johns Hopkins kimeeleza kuwa hadi kufikia sasa, watu 3,098,391 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona kote duniani huku idadi ya vifo vikiwa ni 216,160.

Wakati hilo linatokea, Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mike Pence ameonekana akitembelea kliniki ya Mayo huko Minnesota bila kuvaa barakoa licha ya kwamba kuna kanuni ya kila mmoja kuvaa barakoa.

Bwana Pence anaongoza jopo kazi linaloshughulikia janga la corona katika Ikulu ya rais, Wakati huohuo rais Donald Trump ameagiza viwanda vya kutengenza nyama viendelee na shughuli zao ili kulinda upatikanaji wa chakula wakati janga la virusi vya corona linaendelea.

Rais alizungumzia sheria ya wakati wa Vita vya Korea kuanzia miaka ya 1950 ilipoagiza kwamba mitambo iendelee kutoa huduma.

Aidha, inakadiriwa kwamba wafanyakazi 3,300 wa viwanda vya kutengeneza nyama Marekani wamebainika kuambukizwa virusi vya corona na 20 wamekufa.

Mnamo mwezi  Machi, 2020 Umoja wa Mataifa ulionya kwamba kuhusu tishio la ukosefu wa chakula duniani kote, na Viwanda vya nyama 22 nchini Marekani vimefungwa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.