Star Tv

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari , Dokta Hassan Abbas amesema tayari serikali imepokea Dola Milioni 500 kama mkopo kutoka benki ya dunia ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendeleza sekta ya elimu.

Dokta Abbas amesema hayo leo Aprili 03, 2020 wakati akihojiwa na kituo hiki cha Star Tv katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kenye mada iliyokuwa inaangazia “Ahadi na Uwajibikaji” ambapo amesema kuwa sekta ya elimu kwa Tanzania itaendelea  kufanya vyema kupitia mkopo huo.

Amesema Serikali iliomba mkopo kiasi cha Dola 300 lakini fedha waliyoipata kutoka kwa benki ya dunia ni Dola milioni 500 na kusema  fedha hizo zitasaidia kutumika pia kwenye maboresho ya miundombinu ya elimu.

Kuhusu suala la watoto wa kike wanaopata mimba pindi wanapaokuwa mashuleni amesema sera zilizokuwepo zitaendelea kuimarishwa na kuboreshwa kwa kuendeleza na msimamo wa serikali uliokuwepo isipokuwa ikitokea mwanafunzi amepatikana na mimba shuleni hatafukuzwa lakini pia hatasoma katika shule aliyokuwa akisomea na badala yake ataenda kusoma katika shule nyingine, lengo likiwa ni kumnusuru mtoto huyo kisaikolojia.

Itakumbukwa kuwa mwezi Juni 2017, Rais Magufuli alitangaza rasmi kuwa wanafunzi watakaopata ujauzito hawataruhusiwa kuendelea na masomo katika shule za serikali na baadaye katika taarifa rasmi iliyotumwa kwa barua pepe na moja ya wasemaji wakuu wa benki hiyo aliyopo jijini London, Benki hiyo ilisema Tanzania imenyimwa mkopo wa Milioni 300  iliyoomba kwa ajili ya elimu na inaendelea na majadiliano na serikali kuhusu ya suala hilo.

                            Mwisho.

Latest News

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

RAIS MAGUFULI AKABIDHI TAUSI 25 KWA MAMA MARIA NYERERE NA MARAIS WASTAAFU.
30 May 2020 09:49 - Grace Melleor

Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana I [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.