Star Tv

Familia ya Afisa wa shirika la ujasusi la Marekani (FBI) Robert Levinson, ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha mwaka 2007 nchini Irani amefariki dunia akiwa kizuizini nchini Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump hajathibitisha rasmi kifo chake, lakini amesema kuwa inawezekana kuwa Afisa huyo amefariki dunia.


"Hawajatwambia kuhusiana na kifo chake, lakini watu wengi wanaamini kuwa taarifa hiyo ni sahihi na jambo la kusikitisha"-Rais Donald Trump.


Rais Trump Amesema kwamba taarifa hiyo inatia huzuni kwani Afisa huyo pia alikuwa mgonjwa kwa miaka kadhaa, huku akikiri kwamba alishindwa kumrudisha nchini Marekani kama ilivyopaswa.


Taarifa zinaeleza kuwa familia yake imesema kuwa; "Hivi majuzi tumepokea habari kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao walikuwa wasimamizi wake kwamba mume na baba wa watoto amefariki dunia akiwa kizuizini baada ya kuzuiliwa kwa miaka kadhaa na mamlaka nchini Irani”.

Aidha wanafamilia wansema kuwa sababu au tarehe ya kifo hazikubainishwa ambaye mara nyingi alikuwa akionyeshwa kama mateka wa zamani zaidi katika historia ya Marekani na familia yake imebaini tu kwamba kifo chake kilitokea kabla ya janga la Covid- 19.


                    Mwisho

Latest News

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

“SIJAJA CCM KUTANGAZA NIA”- JOSHUA NASSARI.
08 Jul 2020 15:46 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga [ ... ]

WHO YATOA ANGALIZO JIPYA, USAMBAZWAJI WA COVID-19.
08 Jul 2020 08:41 - Grace Melleor

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba "janga la Corona linaongezeka kwa kasi" na kukiri kwamba "ushahidi unaonye [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.