Star Tv

Jimbo la California limewaamuru wakazi wake kukaa nyumbani wakati wakijaribu kudhibiti maambukizi ya virusi vya coronavirus katika jimbo hilo maarufu zaidi nchini Marekani.

Gavana Gavin Newsom aliwaambia wakazi wa California kuwa watatakiwa kuondoka majumbani mwao kwa  wakati muhimu kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.

Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi.

Kwa ujumla wagonjwa karibu 250,000 kote duniani wamepatikana na virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa kupumua na takriban 9,900 wamekufa.

Gavana Newsom alisema siku ya Alhamis jioni: "Wakati huu tunahitaji kuchukua maamuzi magumu, tunahitaji kutambua hali halisi."

Itawalazimisha biashara ambazo zinaonekana si za lazima kufungwa, huku ikiwaruusu wengine wanaofanya biashara za vyakula na mahitaji na bidhaa nyingine muhimu za nyumbani, maduka ya dawa, benki na vituo vya mafuta ya petroli kuendelea kufunguliwa.

Takribani nusu ya wakazi wa jimbo hilo wamekwishaanza kutekeleza hatua hizo, wakiwemo Jiji la San Francisco.

Gavana Newsom ambaye anatoka chama cha Democratic amesema kuwa sehemu za jimbo hilo zimeshuhudia kuongezeka kwa viwango vya maambuzi ya coronavirus mara dufu kwa kila baada ya siku nne.

Alielezea ubashiri wake katika barua kwa Rais Donald Trump siku ya Jumatano, akitoa wito wa msaada wa haraka kutoka kwa Serikali ya kuu.

Gavana huyo amesema kwa mtazamo wake takribani asilimia 56 ya watu- milioni 25.5 wataathiriwa na virusi vya corona katika kipindi cha wiki nane zijazo .

Hadi sasa California imerekodi visa vilivyo chini kidogo ya 1,000 vya virusi vya corona na vifo 19, kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times.

               Mwisho.

Latest News

KENYA KUTUMA NDEGE CHINA KUCHUKUA VIFAA VYA COVID-19.
06 Apr 2020 15:17 - Grace Melleor

Waziri wa Usafirishaji wa Kenya James Macharia amesema wanatarajia kutuma ndege ya Kenya Airways nchini China siku ya Ju [ ... ]

WAGONJWA WAPYA WANNE WABAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI NCHINI.
06 Apr 2020 14:55 - Grace Melleor

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya uwepo wa ongezeko la wagonjwa wanne wa Corona ambapo watu hao wamepatikana [ ... ]

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALI MJINI LONDON.
06 Apr 2020 06:26 - Grace Melleor

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ya Downing Streeet imeeleza kuwa Waziri huyo amelazwa hospitalini ili ku [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.