Star Tv

Chama cha Mapinduzi CCM kimesitisha shughuli zenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwa ni hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

Ugonjwa huo ulioanzia katika mji wa Wuhan, China Desemba, 2019 na baadaye kuanza kusambaa nchi mbalimbali umesababisha vifo vya watu zaidi ya 4,500 huku Tanzania ikiwa nchi ya tatu Afrika Mashariki kuwa na mgonjwa wa corona baada ya Kenya na Rwanda.

Agizo hilo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Kwa upande mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ameshauri vyama vya siasa nchini Tanzania kusitisha mipango ya kuendesha mikutano ya hadhara ili kupunguza tishio la kusambaa virusi vya corona.

Mbatia ameshauri Serikali kuhakikisha inatoa mwongozo na taarifa mara kwa mara kuhusu hali ya ugonjwa huo pamoja na kuongeza elimu ya uraia kwa raia wanaoendelea kukusanyika.

Mbatia ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam ikiwa ni siku moja baada ya Wizara ya Afya kutangaza rasmi kuingia kwa ugonjwa huo nchini, Mbatia ambaye ni mbunge wa Vunjo amesema tayari ameanza kuchukua tahadhatri hiyo baada ya kisitisha ziara yake Machi 21, mwaka huu katika kata 16 za jimbo hilo. 

              Mwisho

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.