Star Tv

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amethibitisha kisa cha tatu cha maambukizi ya virusi vya corona hapo jana Machi 15, 2020 na kuamuru shule zote nchini humo zifungwe.

Rais Uhuru ameamuru shule zote za kushinda kutwa nzima kufungwa kuanzia siku ya Jumatatu huku shule za mabweni zimepewa muda hadi Jumatano kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea nyumbani kwao kwa sababu ya ugonjwa wa  homa ya Corona pia Vyuo vikuu na vile vya amali vimepewa muda hadi Ijumaa ili kuwapa nafasi wanafunzi wote kurejea kwao.

Kwa mara ya kwanza Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amevunja ukimya kuhusu ugonjwa wa Corona na kuthibitisha kuwa watu wengine wawili wameambukizwa virusi vya corona nchini Kenya achilia mbali kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kilichoripotiwa  siku ya ijumaa Machi 13, 2020 ambapo mtu huyo aliyegundulika   aliwekwa kwenye karantini hospitalini Kenyatta huku wahudumu wa afya wanaendelea kuwatazama walioambukizwa na kuwatibu.

Kutokana na hali hii, wasafiri wanaotokea nchi za kigeni zilizoathiriwa na homa hiyo ya Corona wamepigwa marufuku kuingia ndani ya mipaka ya Kenya na Rais Kenyata amesema watakaoruhusiwa kuingia nchini ni wakenya na wageni walio na vibali rasmi.

Watu 22 wamewekwa karantini ambao wanaaminika kutangamana na mkenya wa kwanza aliyegunduliwa kuambukizwa virusi vya COVID 19 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kulingana na mratibu mkuu kwenye Wizara ya Afya Mercy Mwangangi amesema vituo viwili vya kutoa ushauri nasaha vimeandaliwa kwenye hospitali za Kenyatta na Mbagathi mahsusi kwa walioko kwenye karantini pamoja na familia zao.

Wakati huohuo kaunti ya Mombasa imepiga marufuku vilabu vyote vya densi vya usiku kuendesha operesheni zao kwa siku 30 zijazo, marufuku hiyo ilitangazwa siku ya Jumamosi nagavana Ali Hassan Joho ili kuzuwia uwezekano wa maambukizi ya virusi vya COVID 19.

Aidha, wanaotembelea wagonjwa hospitalini wametahadharishwa kuwa ni watu wawili pekee wa familia watakaoruhusiwa kuwaona waliolazwa, huku kwa sasa makanisa, miskiti na taasisi za kidini zinashauriwa kuhakikisha washirika wao wanapata dawa maalum ya kuosha mikono kadhalika maji na sabuni.

                    Mwisho.

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.