Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein amewataka mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kwanza wa SADC kuhakikisha wanapitisha mikakati imara itakayoweza kuondoa ama kupunguza madhara ya majanga.
Taarifa na Abdalla Pandu.
Rais Shein ametoa agizo hilo kufuatia nchi za jumuiya ya kusini mwa Afrika SADC kupata maafa 160 ambayo yalipelekea zaidi ya vifo elfu 20 pamoja na kuathiri watu zaidi ya milioni 22.
Akifungua mkutano wa kwanza kwa mawaziri wanahusika na masuala ya majanga kwa nchi za SADC Dkt. Shein amesema zaidi ya dola bilioni tatu na milioni 700 zimetumika kwa kipindi cha 2015 mpaka 2018 kukabiliana na majanga yaliotokea hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wan nchi za ukanda wa SADC.
Dkt. Shein amesema kufanyika kwa mkutano huo kumejenga matumaini kwa wananchi wa nchi zote wanachama kwani majanga yamekuwa yakiwapa wasiwasi wa maisha yao na kupoteza watu pamoja na nguvu kazi ya nchi hivyo kuna kila sababu ya washiriki kutekeleza majukumu yao ili kupunguza au kuweza kukabiliana na pia kuvitambua viashiria vya majanga mapema .
Kutokana na mkutano huo kufanyika katika visiwa vya Zanzibar Dkt. Shein amezungumzia uzoefu wa athari za kimazingira kwa nchi za visiwa huku akiwakumbusha kuwa maafa makubwa waliopitia Zanzibar yaliyoyafanya serikali ya Zanzibar kuja na sera na mipango mikakati ambayo baadhi yake imeshatekelezwa.
Waziri wan chi afisi ya waziri mkuu sera bunge kazi ajira vijana na watu wenye ulemavu Jenesta Mhagama amefafanua umuhimu wa mkutano huo katika kuandaa mifumo ya pamoja itakayosaidia nchi za SADC kujiweka tayari na kupunguza madhara ya maafa.
Huku katibu mtendaji wa sadec akifafanua agenda zilizoandaliwa ambazo kupitia mkutano huu wa mawaziri zitajadiliwa na kupitishwa ama vyenginevyo zikilenga mafanikio ya kuziokowa nchi za jumuiya ya kusini mwa Afirika juu ya maafa na majanga mbali mbali.
Mkutano wa SADC ni wakwanza kufanyika Zanziabar na unatarajiwa utakuja na majawabu ya busara katika mchakato mzima wa kujikinga na kukabiliana na maafa yakiwemo yanayotokana na watu au ya kiasili kwa nchi zote wanachama.
Mwisho