Star Tv

Jeshi la Polisi Nchini limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 504 wa matukio mbalimbali ya uhalifu akiwemo Mganga wa kienyeji Itawa Mwanamiwa na mwenzake Tabu Mwanduru ambao waliwaaminisha watu kuua Wanawake 50 na kuwabaka ili kupata utajiri hali iliyopelekea Wanawake 29 kuuwawa na kubakwa katika maeneo ya Wilaya za Kwimba,Misungwi na Mkoa wa Shinyanga.

Taarifa na Salma Mrisho

Operesheni iliyofanywa na Polisi kuanzia tarehe 03.02.2020 na hadi kufikia february 14 ambayo imekamata watu wanaotekeleza vitendo vya mauaji,wakata mapanga,kufanya uganga bila kibali,unyang'anyi wa kutumia silaha na kadhalika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Operesheni Maalum Za Jeshi la Polisi Mihayo Mskela amesema tukio la Mganga Itawa baada ya kukamatwa na kuhojiwa imebainika kuhusika na mauaji hayo na kuwataja washirika wao 17 ambao ni wakata mapanga na wanaendelea kuhojiwa.

Mkoani Tabora amekamatwa Buhimila Mapembe kwa tuhuma za kutumia fimbo maalum kuwaaminisha wateja wake ambao ni wakata mapanga kuwakinga na nguvu ya sheria na kutokana na imani hiyo imepelekea askari polisi wawili wa kituo cha polisi Ngaruka Mkoa wa Kigoma na askari mmoja wa suma jkt na askari mgambo wa mkoa wa tabora kuuwawa na kuchukuliwa sehemu zo a siri kwa ajili ya dawa.

Ameendelea kusema kuwa kikosi maalum cha anti Homicide kinachoendelea kufanya operesheni ya wakata mapanga Mkoani Geita kimefanikiwa kukamata wauaji halisi wanne na operesheni hii imefanikiwa kupatikana kwa watuhumiwa wa wizi wa Mifugo ambapo jumla ya Ng’ombe 105 wamepatikana.

Operesheni hiyo imefanyika katika mikoa ya Geita,Kagera,Mwanza,Shinyanga,Simiyu na Tabora.

                                                                      Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.