Star Tv

Mwili wa aliyekuwa waziri wa viwanda na baishara katika serikali ya awamu ya tatu Idd Simba umezikwa Ijumaa hii jijini Dar es salaam huku baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakizungumzia uchapa kazi na uthubutu wake katika kuleta maendeleo wakati wa uhai wake.

Taarifa na Athuman Mihula.

Ni safari ya mwisho ya Idd Simba ambaye anakumbukwa kwa mengi aliyofanya katika ujenzi wa Tanzania hasa pale alipopewa dhamana ya kuwa waziri wa viwanda na biashara wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwa upande wao viongozi wa dini nao walipata nafasi ya kuelezea mazuri yaliyofanywa na Idd Simba ikiwemo uchapa kazi wakuleta maendeleo wakati wa uhai wake.

Idd Simba aliyezaliwa mwaka 1935 na kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es salaa mwaka 1995 hadi 2005 na kupata kuhudumu katika nafasi ya waziri wa viwanda na biashara amefariki dunia Februari 13 mwaka huu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa akipatiwa matibabu.

                                                                        Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.