Star Tv

Marekani imetangaza kufikia makubaliano ya kupunguza ghasia kwa siku saba nchini Afghanistan ambayo inatumai yatawezesha kupatikana kwa mkataba wa amani na kundi la Taliban.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper, ametangaza kufikiwa kwa makubaliano hayo baada ya mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO uliofanyika mjini Brussels, ikiwa ni siku moja baada ya Rais Ashraf Ghani wa Afganistan kusema kuwa mazungumzo kati ya Marekani na Taliban yamepiga hatua muhimu.

Esper amesema  Marekani na kundi la Taliban zimejadiliana kuhusu pendekezo la siku saba la kupunguzwa kwa ghasia na kwamba leo wanashauriana na washirika kuhusu pendekezo hilo na kumekuwa na mikutano kuhusu mwelekeo utakaofuata.

Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani hakusema ni lini hasa makubaliano hayo yataanza kutekelezwa, lakini afisa mmoja wa kundi la Taliban ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi hilo litaanza kupunguza mashambulizi yanayotokana na shughuli zake za kijeshi kuanzia siku ya leo.

                                                                 Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.