Star Tv

Ndole ni kijiji ambacho kipo pembezoni mwa Wilaya ya Mvomero katika milima ya Ndole, wakazi wa kijiji hicho wengi wao  wakijishughulisha zaidi na kilimo cha mazao ya Ndizi, maharage pamoja na magimbi ambayo yamekuwa yakisafirishwa sehemu mbalimbali nchini.

Licha ya kujituma katika uzalishaji wa mazao lakini kwa sasa wanakatishwa  tamaa kutokana na adha ya usafiri unaosababishwa na kubomoka kwa daraja linalounganisha kjiji hicho na vijiji jirani hata kupelekea magari kushindwa kutoka au kuingia ndani ya kijiji hicho.

Wafanyabiashara na madereva wa magari nao wanakumbwa na changamoto hiyo ya kubomoka kwa daraja  hatua inayowalazimu kuzunguka umbali mrefu kuingia kijijini hapo kupitia Gairo  pamoja na Kibati.

Uongozi wa kijiji cha Ndole kupitia kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho Adrian Paulo  amesema mamlaka husika inayohusika na ujenzi wa miundombinu wamepewa taarifa kuhusu adha hiyo lakini wanashangazwa na ukimya uliopo,

Wakati bado wananchi hao  wanasubiri ufumbuzi  wa  ujenzi wa daraja hilo, vijana wa kijiji hicho watengeneza  mfano wa daraja dogo la miti ambalo nalo si salama  kutokana na kuhitaji umakini mkubwa wakati wa kupita  hasa kwa wale wanaotumia usafiri wa pikipiki.

Licha ya kuwa ni hatari lakini si haba kutokana na mizigo mingi kupitishwa na pikipiki kupitia mfano huo wa daraja hilo, huku magari yayotoea maeneo ya Dumila,Turiani na Morogoro yakiishia ng’ambo na  yale yanayotoka  kijijini hapo nayo yakiishia ng’ambo ya pili ya mto.

Serikali ya wilaya Mvomero imekirii kutambua uwepo wa changamoto hiyo ya kubomoka kwa daraja inayaokawabili wakazi wa kijiji cha Ndole na wako kwenye mchakato wakulitengeneza.

Kwa mara ya Kwanza Daraja hilo limebomoka mwezi wanne mwaka 2019, ambapo mpaka sasa limejengwa zaidi ya awamu tatu lakini  awamu hizo zote limekuwa likibomelewa na mvua na hivyo kupelekea changamoto ya usafiri kusuasua hatua ambayo inatajwa kurudisha nyuma maendeleo ndani ya kijiji hicho kutokana na idadi ya watu wanaoingia kupungua huku wananchi nao wakishindwa kusafirisha mazao yao kwenda sokoni na hivyo  kupelekea mazao mengi kuharibika na wengine kuamua kuuza kwa bei ya chini.

 Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.