Star Tv

Polisi kitengo cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikiwa kupunguza matukio ya ajali za barabarani hadi kufikia asilimia thelathini na tano kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi mwishoni mwa mwaka 2020.

Taarifa na Dickson Kanyika.

Mwaka 2015 serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na shirika la afya Duniani ( WHO ) chini ya Ufadhili wa Bloomberg,  ilianzisha programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanahabari ikilenga kufikisha elimu kwa jamii kote nchini ili kudhibiti matukio ya ajali.

Kwa kiasi kikubwa mafanikio yamepatikana kutokana na kupungua kwa ajali hususani katika mikoa ya Kaskazini na kusini mwa tz, anasema Marry kessy Mratibu wa Programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanahabari.

Sanjari na maelezo ya Marry kessy,  Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania Fotunatus Muslimu alinukuliwa na chombo kimoja cha habari jijini Dar es salaamu akithibitisha kwamba ajali za barabarani zimepungua kwa zaidi ya asilimia 35 nchini humo, Hii ni kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya wadau wa usalama barabarani , vyombo vya habari na jeshi la polisi.

Pamoja na hatua hii nzuri iliyofikiwa lakini bado wadau wameshauri kuendelelea kushirikisha wanahabari,  na kubwa Zaidi ikieleza  ni kufanyika maboresho kwenye sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 ambayo inatajwa kuwa kikwazo cha kupunguza ajali nchini kutokana na mapungufu makubwa yaliyoko kwenye sheria hiyo.

Mwaka 2018 Shirika la afya duniani WHO lilitoa ripoti mpya iliyoonesha zaidi ya watu mil.1.35 wanapoteza maisha kila mwaka, huku wengine zaidi ya mil.20 hadi 50 huachwa wakiwa majeruhi, huku nchini Tanzania kikubwa kinachopigiwa kelele kwa sasa ni kufanyiwa marekebisho kwa sheria ya usalama barabarani ambayo imeonekana kuwa na mapungufu makubwa.

                                                     Mwisho.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.