Star Tv

Afisa mkuu wa tiba nchini Uingereza amesema mgonjwa wa nne aliyeambukizwa virusi vya corona amegunduliwa nchini humo ambapo kugunduliwa kwa mgonjwa huyo kumetokea baada ya kufuatia kisa kilichokuwa kinafuatiliwa na wataalamu baada ya kubainika kwamba mgonjwa huyo alikuwa ametangamana na mtu mwingine aliyepata virusi hivi nchini Ufaransa.

Hii imetokea baada ya raia wa Uingereza na wengine wa kigeni karibia 200 kuhamishwa kutoka mji wa Wuhan kwa ndege ya mwisho ya Uingereza ambayo iliwasili katika uwanja wa ndege wa RAF Brize Norton leo Jumapili.

Idadi ya waliokufa kwa virusi vya corona kwa sasa inatajwa na wataalamu wa afya kuwa juu zaidi kuliko idadi ya waliokufa kwasababu ya virusi vya Sars mwaka 2003, kulingana na maafisa wa afya nchini Uchina.

Katika taarifa iliyotolewa leo Februari 2,2020 na Profesa Chris Whitty ambaye ni afisa mkuu wa tiba Uingereza, amesema kwamba mgonjwa huyo wa wa hivi karibuni kutokea nchini humo amehamishwa hospitali ya kitaifa ya Royal Free hospital kaskazini ya Uingereza.

Ofisi ya mambo ya nje imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa ya pili na ya mwisho kutoka kwa serikali kuchukua wale waliokwama katika mji wa Wuhan kitovu cha virusi ipya vya corona.

Waliobebwa na ndege hiyo ni pamoja na raia 105 wa Uingereza na familia zao pomoja na raia 95 wa Ulaya. Pia wafanyakazi 13 na wahudumu wa afya walikuwa kwenye ndege hiyo.

Waliohamishwa wamepelekwa eneo la Milton Keynes na watawekwa katika karantini kwa siku 14 ili kuchunguzwa afya zao.

Balozi wa Uingereza Beijing, Dame Barbara Woodward, ameiambia BBC kwamba raia wawili wa Uingereza waliotaka kujumuishwa kwenye safari hiyo walizuiliwa baada ya joto la mwili kuwa juu wakati wa ukaguzi nchini Uchina.

Mwanamume huyo amelazwa katika hospitali ya Palma Ijumaa, pamoja na mke wake na binti zake wawili. Familia yake nyengine wamebainika kwamba hawajaambukizwa virusi hivyo.

Wizara ya afya imesema inachunguza uwezekano wa yeyote ambaye huenda alitangamana na mwanamume huyo

Zaidi ya raia 100 wa Uingereza na familia zao wamehamishwa hadi Uingereza kwa ndege zilizosimamiwa na serikali na nchi zingine.

                                                                                                    Mwisho.

Latest News

OPARESHENI YA KUSAKA WAHALIFU NCHINI:Watuhumiwa 504 wakamatwa na polisi.
14 Feb 2020 18:00 - Grace Melleor

Jeshi la Polisi Nchini limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 504 wa matukio mbalimbali ya uhalifu akiwemo Mganga wa kienyej [ ... ]

KUSHUGHULIKIA MASUALA YA MUUNGANO:Dkt Shein amhakikishia Zungu ushirikiano.
14 Feb 2020 17:48 - Grace Melleor

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemuhakikishia Ushirikiano Waziri wa Nchi [ ... ]

BURIANI IDDI SIMBA:Umati mkubwa wajitokeza kumzika jijini Dar es Salaam.
14 Feb 2020 17:21 - Grace Melleor

Mwili wa aliyekuwa waziri wa viwanda na baishara katika serikali ya awamu ya tatu Idd Simba umezikwa Ijumaa hii jijini D [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.