Star Tv

Watu 73 walifariki jana nchini China bara kutokana na homa ya virusi vya corona, na kufikisha idadi ya vifo vya maradhi hayo kufika 563.

Zaidi ya asilimia 80 ya vifo na maambukizi nchini China vinatokea katika mkoa wa Hubei ilikoanzia homa hiyo hatari. Hadi wakati huu watu wawili wameuawa na maradhi ya hayo nje ya China Bara, mmoja nchini Ufilipino na mwingine katika kisiwa cha Hong Kong, na wahanga wote hao walikuwa wameutembelea mji wa Wuhan ambao ni chimbuko la ugonjwa huo.

Kitisho cha ugonjwa huo kinaripotiwa kuongezeka katika meli ya anasa ya kijapani iliyozuiliwa katika bandari ya Yokohama, ambapo wizara ya afya ya Japan inasema watu 20 kati ya 3,700 waliomo ndani ya meli hiyo iliyowekwa katika karantini, wamethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

                                                                                    Mwisho.

Latest News

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

“SIJAJA CCM KUTANGAZA NIA”- JOSHUA NASSARI.
08 Jul 2020 15:46 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga [ ... ]

WHO YATOA ANGALIZO JIPYA, USAMBAZWAJI WA COVID-19.
08 Jul 2020 08:41 - Grace Melleor

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba "janga la Corona linaongezeka kwa kasi" na kukiri kwamba "ushahidi unaonye [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.