Star Tv

Wanafunzi zaidi ya 2700 wa shule ya msingi Bangulo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam wanalazimika kutumia matundu ya vyoo nane tu hali inayotajwa kuwapa shida wanafunzi hao wakati wanapohitaji kujisaidia huku shule hiyo ikiwa na jumla la madarasa 14 pekee ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi  shuleni hapo

Habari na Adam Damian.

Linaposikika jijini la Dar es salaam katika fikra na nafsi za watu wengi hasa walio nje ya jiji hilo hudhani pengine halikabiliwi cha changamoto kama vile upungufu wa madawati, shida za maji, vituo vya afya, au miundombinu.

Lakini hali ni tofauti katika wilaya ya Ilala ambako shule ya msingi ya Bangulo yenye wanafunzi zaidi 2700 inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo, upungufu wa walimu na uchache wa madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzo katika shule hiyo

Wananchi wa mtaa huo wamepaza sauti zao kutaka msaada wakisema kuwa hali ni mbaya katika shule hiyo yenye madarasa 14 tu na matundu nane ya vyoo

Aidha wakazi wa maeneo hayo wameiomba serikali kutazama suala hilo kwa jicho la huruma ili waweze kutatuliwa changamoto hizo huku ikiwaomba viongozi wawe na tabia kutembelea maeneo hayo ili kujua shida na changamoto zinazowakabili shule kama ilivyo shule hiyo ya msingi ya Bangulo

Kwaupande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Bangulo Mwele Gudluck amekiri kuwepo kwa changamoto hizo huku akibainisha kuwa serikali ni sikivu hivyo kero zote zitatatuliwa haraka ili kutoa fursa kwa wanafunzi shuleni hapo kupata elimu katika mazingira rafiki

Aidha, kwa upande mwingine imeelezwa kuwa mtaa wa Bangulo hauna kituo cha polisi huku kukiwa na mikakati ya makusudi ya kujenga kituo hicho ili kudhibiti matukio ya uhalifu

 

                                                                          Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.