Star Tv

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameamuru Mhandisi mshauri anayesimamia  mradi wa ujenzi wa chuo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA mkoa wa Rukwa pamoja na mkandarasi wakamatwe na kuwekwa ndani kwa muda usiojulikana kutokana na kushindwa kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa wakati  licha ya kuongezewa muda.

Taarifa yake;Brown Lawi Mtawa.

Maagizo ya kukamatwa kwa  mhandisi mshauri   pamoja na mkandarasi  wa  Tenda Company ltd yametolewa na Prof. Ndalichako baada ya kukagua  ujenzi wa chuo cha VETA  na kuona ujenzi huo  bado  unasuasua.

“Kwahiyo akakae ndani mpaka vile vifaa ulivyoruhusu hapa vitakaporudi ndio mumuachie kwasababu naona sasa hii itakuwa ni kuchezeana, majibu  yanayoeleweka hakuna unayonipa siwezi kuwa nakuja kila siku natoa maelekezo  hayatekelezwi” -Prof.Joyce Ndalichako-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

Kwa upande wao baadhi ya  wafanyakazi katika chuo hicho wameeleza changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapokuwa katika ujenzi wa chuo hicho cha ufundi.

“Mnaweza mkapangiwa kazi lakini mkimaliza kazi mapema mnaongezewa kazi baada ya kuona kwamba hawa watu hawajachoka hata ikiwa ni saa sita usiku mnapewa elfu sita ileile”-Simon Mateo – Mfanyakazi wa Kibarua Tender company ltd.

Kukamilika kwa chuo  hicho cha VETA kutasaidia kuleta mafanikio  kwa wakazi wa Rukwa  na taifa kwa ujumla katika  kuijenga Tanzania ya viwanda kwakuwa kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafuzi zaidi ya 1500 kwa mwaka katika kada tofauti.

                                                                                                              Mwisho.

 

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.