Star Tv

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya juhudi kuendeleza miradi ya maji safi na salama ambayo itawezesha changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kuwa historia.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameyasema hayo leo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mkoa wa Mjini Magharibi (ZUWSP)-ADF 12 huko Saateni Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni shamrashamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dk. Shein amesema kuwa huduma za maji safi na salama kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 zilikuwa zikitolewa kwa ubaguzi licha ya kuwa ni neema aliyoileta MwenyeziMungu kwa waja wake.

“Matumaini yangu ni makubwa kwa mradi huu, fedha zote lengo lake ni kuhakikisha kwani mikakati kabambe yakuimarisha miradi ya maji imeaanza  natumai awamu zijazo zitaendeleza mikakati hiyo kwa azma ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu hapa nchini, nasisitiza kuwa maji hayauzwi hapa Zanzibar bali yanachangiwa”.

Alisema kuwa kwa Zanzibar wakati huo huduma zote muhimu zilianza katika nyumba za mawe zilizokuwepo katika eneo la mji mkongwe pekee yake.

Rais Dk. Shein alieleza umuhimu wa maji kwa wanaadamu, wanyama na miti na kueleza kuwa ndio maana serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikafanya juhudi za makusudi kuhakikisha huduma hiyo inaimarika hasa ikizingatiwa kuwa maji hayana mbadala.

Aidha, Rais Dk. Shein ameeleza jinsi ya Washirika wa maendeleo wakiwemo nchi rafiki ikiwemo Ras al Khaimah, Sharja, Japan, China, India  na wengineo walivyoiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maji.

Mara baada ya kuwasili katika eneo la Saateni, Rais Dk. Shein amepata maelezo juu ya mradi wa maji  kwa tanki la Saateni na tanki la mnara wa mbao kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Mussa Ramadhan Haji.

Akisoma taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Ali Halil Mirza ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein kwa uongozi wake mahiri kwa kuamua kutekeleza Mradi wa Maji na Usafi wa Maziringira wa Mkoa wa Mjini Magharibi.

“Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati inatarajia  mradi huu utaendeshwa na kutunzwa vizuri kwa ushirikiano kati ya mamlaka ya maji Zanzibar, tujitahidi kuutunza.”-Ali Halil Mirza-Katibu Mkuu   Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati.

                                                                                                Mwisho.

 

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.