Star Tv

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Muliro Jumanne amekanusha taarifa zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa kuna wanachama hao wa CHADEMA wametekwa jijini Mwanza.

Muliro amesema hakuna utekaji uliotokea bali wanachama hao walikamatwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema wa mtaa wa Mahina.

Kamanda Muliro, akizungumza na waandishi wa habari amesema baada ya kupatikana taarifa zilizokuwa zibainisha kuwa siku ya Disemba 29, Mwaka huu Majira ya 15:00 mtaa wa Mahina Kata ya Mahina wilayani Nyamagana kulipatikana taarifa toka kwa raia wema kuwa kumeonekana watu wawili waliohisiwa kuwa siyo watu wema wakiwa karibu na Hoteli ya Paradise.

“Jeshi la polisi  lilifanya ufuatiliaji wa haraka na kufika eneo hilo na kuwakamata watu hao wawili, ambao katika mahojiano ya awali walikataa kutoa utambulisho wao kuwa wamefika maeneo hayo kufanya shughuli gani”, Amesema ACP Muliro.

Amesema baada ya wanachama hao kukamatwa walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi cha kati na kutoa ushirikiano kwa askari pia kutaja majina yao kuwa ni Abdukarimu Muro (31),  ambaye ni afisa habari wa katibu mkuu CHADEMA Mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam na Said Haidani (30), Dereva wa katibu mkuu CHADEMA, Mkazi wa Mbezi Kimara Dar es Salaam wameambatana na Katibu Mkuu CHADEMA, Mh. John Mnyika pamoja  na polisi waliwaachia huru baada ya kujiridhisha hawakuwa wahalifu.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limetoa onyo kwa  watu wasiokuwa na taarifa rasmi na wenye tabia ya kuzusha mambo hasa  watu wanapokamatwa kwa kusema wametekwa waache tabia hiyo.

Aidha,amesema hali hiyo yakutoa taharuki ininazusha taharuki kwa jamii na kwa kufanya hivyo ni makosa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi  watakapobainika.

 

 Mwisho.

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.