Star Tv

Kamati ya kudumu ya bunge ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi,kifua kikuu na dawa za kulevya  inatarajiwa kufanya kikao Maalum Jijini Mwanza cha kutangaza azimio la viongozi wa dini katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa Kifua Kikuu Nchini.

 Taarifa Hii na Mwanahabari wetu Sudi Shaban..

Inaelezwa kuwa Ugojwa wa Kifua Kikuu uneendelea kuwa tishio la kiafya nchini, ikiwa Zaidi ya watu elfu 60 kwa Mwaka wanaugua Ugonjwa huu.Mkutano huu ni sehemu ya kuainisha yakuwa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu yanaendelea na njia ya kuutotokomeza kabisa ikiwa zinatafutwa.

Kambi rasmi ya wabunge Bungeni ya kupambana na ugojwa huo walibaninisha novemba 30 mwaka huu kwamba kunatarajiwa kikao cha kutangaza maazimio ya viongozi wa dini ya mapambano ya Kifua Kikuu.

Tafiti za masuala ya kiafya zinabainisha kuwa kila Mgonjwa Mmoja wa Kifua Kikuu ambaye hajapata Matibabu huambukiza watu 2O Kwa Mwaka.

Katika hatua Nyingine imetajwa tathmini ya maandalizi ya Siku ya Uhuru Desemba 9  mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza ambapo sherehe za Miaka 58 ya uhuru itafanyika katika viwanja vya CCM Kirumba na Maandalizi yake yametajwa kuwa  sio haba.

Sherehe hizo zitaongozwa na Kauli Mbiu Isemayo Miaka 58 ya uhuru na Miaka 57 ya “Jamhuri, Uzalendo, Uwajibikaji na ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Taifa Letu”.

 

                                                                                                                        Mwisho,

 

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.