Star Tv

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amelipongeza bunge kwa kupitisha sheria ya madini inayoelezea mali kama madini kuwa ni mali ya watanzania .

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kahama ambapo ameiongeza kampuni ya Barrick ambayo imekubali kuingia ubia na Tanzania kwa kuunda kampuni inayoitwa twiga kwasasa.

 Amesema fedha zitakazopatikana kutokana na sekta hiyo ya madini zitaweza kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi kama vile suala la maji, elimu na huduma ya kupata tiba bora.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli ametoa onyo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutokwenda kukopa pesa benki kwa ajili ya miradi iliyopo katika wilaya zao.

“Na hii ni kwa wakurugenzi wote Tanzania sitaki kuona halimashauri yoyote inakwenda kukkopa hela kwenye benki, na wale ambao wamezikopa wavunje hiyo mikataba.”

Rais Magufuli amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi walioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika novemba 24, mwaka huu na kusisitiza mshikamano kwa wananchi ili kuleta maendeleo kwa taifa.

 

                                                                                                  Mwisho.

Latest News

RAIS TRUMP ASHUTUMIWA KUWAGAWANYA RAIA WAKE.
04 Jun 2020 10:28 - Grace Melleor

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amemshutumu Rais Donald Trump, kwa kuleta mgawanyiko na kutumia viba [ ... ]

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.