Star Tv

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wanachama wa chama hicho kuunganisha nguvu katika kudai uchaguzi huru na haki pamoja na tume huru ya uchaguzi.

 Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya chama hicho na vyama vingine saba vya upinzani kutangaza kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma.

 Lipumba amewataka wanachama wa CUF kutokata tamaa kwa yote yaliyojitokeza kwenye mchakato huo.

 Mwenyekiti huyo wa CUF ameitaka kamati ya utendaji ya taifa kuendelea na kazi ya kuandaa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 itakayojipambanua katika sera za haki na usawa .

Wakati Prof. Lipumba akitoa msimamo huo wa CUF, bado kuna mazungumzo ya ndani baina ya vyama vya siasa vya upinzani vilivyojitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, mazungumzo ambayo bado haijajulikana hatima yake.

                                                                                    Mwisho.

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.