Serikali imesema itahakikisha sekta ya usafiri wa anga nchini inaimarika ikiitaka mamlaka ya ufasiri wa anga nchini TCAA kuongeza uwajibikaji zaidi ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa ubora kama ilivyo kwenye mataifa yaliyoendelea.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa udhibiti wa uchumi na biashara wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA Daniel Malanga, wakati wa mkutano uliowakutanisha kamati maalumu ya usafiri wa anga ya jumuiya ya Afrika mashariki na sekretaieti ya jumuiya hiyo unaokusudua kujadili changamoto zinazokabili mamlaka hizo na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuboresha sekaya ya usafiri wa anga.
Aidha, TCAA imesema kuwa itahakikisha inaongeza vyanzo vya mapato na kuondokana na kutegemea zaidi mapato yanayotokana na maegesho ya ndege.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamesema kutakuwa muhimu sana katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi za jumuiya hiyo nakuongeza ufanisi wa huduma za usafiri wa anga Afrika ya mashariki
Kamati hiyo hukutana kila baada ya miezi sita ikiwa ni muendelezo wa kutatua changamoto na kuweka mikakati kadhaa ili kuhakikisha mamlaka za usafiri wa anga kwa nchi za Afrika mashariki zinaimarika zaidi
Mwisho