Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe  Magufuli ametunukiwa  shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa katika sayansi kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametunukiwa shahada hiyo leo Alhamisi Novemba 21, 2019 katika mahafali ya 10 ya chuo hicho ambapo mkuu wa chuo hicho Rais mstaafu, Benjamin Mkapa naye amehudhuria katika mahafali hayo.

Viongozi waliohudhuria mahafali hayo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, mawaziri kutoka wizara mbalimbali pamoja na wabunge.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema shahada hiyo inatolewa kwa Rais Magufuli kutokana na uongozi wake katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kuwekeza katika elimu, miundombinu, mawasiliano, nishati, utalii na kuimarisha utawala bora pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.

Prof. Faustine amesema shahada hiyo imewahi kutolewa kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010 na pia waziri mkuu wa zamani marehemu Rashid Kawawa ambapo Rais Magufuli ni kiongozi wa tatu kutunukiwa shahada katika chuo cha UDOM.

 Wahitimu 6,488 watatunukiwa astashahada, shahada, stashahada ya juu, shahada ya umahiri na shahada ya uzamivu.

 

                                                                            Mwisho

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.