Wananchi wa kata tatu za Matambalale ,Namikulo na Namileme wilayani Ruangwa mkoani Lindi wamelipwa fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4 ili kupisha mradi mkubwa wa uchimbaji madini aina ya Bunyu
Mgodi huo unaomilikiwa na Lindi jumbo ni miongoni mwa migodi sita ya uchimbaji madini aina ya Bunyu wilayani humo .
Baadhi ya wananchi waliolipwa fidia ili kupisha uchimbaji huo wameiomba serikali iwape kipaumbele cha kupata ajira pindi mgodi utakapoanza kufanya kazi
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashimu Mgandilwa amewataka wakazi wa wilaya hio kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa pindi watapo tangaza nafasi za ajira
Mgodi huo wa uchimbaji madini aina ya Bunyu utakapo kamilika unatarajiwa kuajiri zaidi ya watu elfu tatu
Mwisho