Star Tv

Wakulima 170 wa kitongoji cha Lyahamile Mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa  wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wameachwa njia panda baada ya serikali ya wilaya hiyo kuwapiga marufuku kuendelea na shughuli za kilimo katika shamba la Mpunga la Katenge kwa madai kuwa eneo la Shamba hilo lina mgogoro.

Lyahamile ni moja ya kitongoji kilichopo mtaa wa Nyelegete katika mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa halmashauri ya wilaya ya Mbarali.

Kwa asilimia 100 ya wakazi wa eneo hilo wanategemea kilimo cha zao la Mpunga na Ufugaji katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Kataka kipindi hiki cha kuelekea msimu wa kilimo, wakazi hawa wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea walaka wa serikali ukiwataka kuto jihusisha na kilimo cha mpunga katika shamba hilo.

Katazo hilo la mkuu wa wilaya limekuwa kitendawili kwakazi hao, kwani wanadai kuwa kwa miaka mingi wamekuwa wakitegemea mashamba hayo kuendesha maisha yao.

Star TV imezungumza kwa njia ya simu na mkuu wa wilaya ya Mbarali Ruben Mfune,  kutaka kupata ufafanuzi juu ya sababu hasa ya serikali kupiga marufuku shuguli za kilimo katika shamaba hilo.

“Kilichotokea ni kwamba baadhi ya watu wanafanya lile eneo kwamba wao ndio wamiliki badala yakuwa eneo la umma na ndio maana sikutaka mtu yeyeto alitumie kwasababu baadhi yao wanalitumia kwa manufaa yao wao wenyewe”

Migogoro ya kugombea ardhi wilaya ya Mbarali ni moja ya changamoto kubwa inayotajwa kuendelea kurudisha maendeleo ya wananchi nyuma, huku migogoro hiyo ikielezwa kuchochewa zaidi na viongozi waliopewa mamlaka kuwaongoza wananchi.

                                                                Mwisho.

 

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.