Star Tv

Mwandishi wa Habari za ,uchunguzi Erick Kabendera àmeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa amepata huduma za Kitabibu katika Hospitali ya Amana na katika uchunguzi wa awali uliofanyika madaktari wamebaini kuwa anamatatizo katika pingili za mgongo.

Amedai kuwa Septemba 17,2019 alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambapo alifanyiwa vipimo vya X-ray, damu pamoja na vipimo vingine lakini bado anasubiri majibu ili apatiwe màtibabu. Kabendera amedai kuwa bado ana maumivu makali na vipimo zaidi vimefanyika ili kubaini kama ana matatizo zaidi na majibu yake atapewa mwishoni mwa wiki hii Mshtakiwa Kabendera ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Rwezile wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa upelelezi bado haujakamilika Baada ya kueleza hayo wakili wake Jebra Kambore ameuomba upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba mosi mwaka huu mshtakiwa amerudishwa rumande. Katika kesi hiyo,Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh milioni 173. Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida. Shitaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Katika shitaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakatisha fedha sh.173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu.

Latest News

ZANZIBAR YAFUNGUA MILANGO KWENYE UTALII.
06 Jun 2020 10:30 - Grace Melleor

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya [ ... ]

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.