Star Tv

 

Jumla ya watuhumiwa sita wa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya  Katoro  ya Islamic seminari  kwa  kumtuhumu  kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja  Mudy Muswadiku aliyekuwa na umri wa miaka kumi na tisa  wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa mara ya kwanza. Watuhumiwa hao ni  mlinzi wa shule  ya sekondari ya Katoro ya  Islamic Seminari  Badru Tibagililwabe, Majaliwa Abdul ambaye ni  mwalimu shuleni hapo, pamoja na wanafunzi wanne ambao wanashtakiwa kwa  tuhuma za kumpiga na kisha kumsababishia kifo cha  Mudy Muswadiku mwanafunzi wa kidato cha nne mnamo tarehe 4 Aprili mwaka huu. Watuhumiwa hao wamefikishwa   mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Bukoba  Frola Kaijage na kusomewa kesi ya mauaji namba 18 ya mwaka 2019 na kaimu mkuu wa mashtaka mkoa wa Kagera wakili Chema Maswi ambaye aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi bado unaendelea.

Hakimu mkazi Frola Kaijage amewataka watuhumiwa hao kutojibu chochote kutokana  na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Kesi hiyo imehairishwa hadi Septemba kumi na sita mwaka huu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.