Star Tv

Pamoja na Serikali kupiga marufuku uvamizi wa misitu katika Msitu wa Rwamgasa na Geita bado baadhi ya Wananchi wamekaidi na wengine kufikia hatua ya kukata maeneo ya misitu na kuuza kwa Wananchi kwa elfu hamisini wakiwaaminisha kuwa maeneo hayo yatapimwa na yatakua mali yao.

Wilaya ya Geita Ina hifadhi tatu za misitu ambayo ni Geita, Rwamgasa na Usindakwe zende jumla ya hekta 79,446. Huku hali ya misitu ikionekana kutokuridhisha kutokana na changamoto mbalimbali za uvamizi na uharibifu kwa shughuli za kilimo, malisho ya mifugo, ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji mkaa na matimba yanayotumika kwa uchimbaji. Katika msitu wa Geita baadhi ya Wananchi wanaishi na kuendelea na shuguli zao pamoja na kutolewa mara kadhaa lakini wanarudi.

Baadhi ya Wananchi wanaokaa eneo hili waliamua kuuita uongozi wa Mtaa wakidai wamekua wanafanyiwa fujo na kutaka ulinzi ndani ya hifadhi ya msitu huu. Kwa mujibu wa sheria za misitu hairuhusiwi kufanya shughuli zozote ndani ya misitu. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amesema "ukikutwa unakata miti utakamatwa na utalipa miti yote na kusisitiza kuwa waliomo katika maeneo yote ya hifadhi ya misitu waondoke".

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.