Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewahukumu kifungo cha miaka 18 jela ama kulipa faini ya shilling million 315 raia kutoka nchini China kwa kukutwa na viroba tisa vyenye mchanga na boksi moja la madini wakisafirisha katika gari namba KBW 515 Toyota land Cruiser.
Kufuatia mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP kutoa kibali cha kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi na kukutwa na madini kinyume cha sheria Raia watatu wa China. Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewatia hatiani watu hao watatu kwa makosa mawili kila mmoja na kuwahukumu kifungo cha miaka 18 ama kulipa faini ya shilling millioni mia tatu kumi na tano za Kitanzania huku gari walilokuwa nalo aina ya lend Cruiser namb KBW 515 L likitaifishwa.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo mheshimiwa Veronica Mgendi amesema kuwa washitakiwa hao watatu kwa pamoja walitenda makosa hayo kinyume cha sheria za nchini hivyo adhabu hiyo liwe fundisho. Awali wanasheria wa serikali wametoa maelezo ya shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo wakisema kuwa washitakiwa hao watatu kwa pamoja wilayani Tarime walikuwa na gari ambalo limesheheni mali hiyo kinyume cha sheria. Mnamo tarehe 12/6/2019 raia hao walikamatwa Nkenge wilayani Tarime wakiwa na mchanga kilo 3.75 wa madini ya aina mbali mbali wakiyasafirisha bila kibali.