Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Msumbiji wameishambulia serikali kutokana na kile walichosema ni kushindwa kwa serikali hiyo kuzuwia wapiganaji wa itikadi kali ya Kiislamu kuvuruga eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, wakidai mamia ya raia wamepoteza maisha.
Askofu wa jimbo la Pemba na rais wa tume ya haki na amani ya baraza la maaskofu, Dom Luiz Fernandes, amewashutumu maafisa wa kitaifa na jumuiya ya kimataifa kwa kutofanya vya kutosha kuzuwia wimbi la mashambulizi ambalo amelifananisha na kimbunga. Matamshi yake yamekuja wiki kadhaa kabla ya ziara ya mwezi Septemba nchini Msumbiji itakayofanywa na kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis kama sehemu ya ziara ya mataifa ya Afrika ambayo pia itamfikisha Madagascar na Mauritius.
CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW.