Star Tv

Wizara ya mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha taarifa ya kuwepo kwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola, siku ya Jumapili, katika mji ulio mashariki mwa nchi hiyo wa Goma wenye takribani wakazi milioni 1.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, mtu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo ni kiongozi wa kidini ambaye aliambukizwa akiwa ziarani mjini Butembo ambapo alichangamana na watu waliokuwa na maambukizi ya ugonjwa wa ebola. Kuripotiwa kwa kisa hicho, kumeibua hofu ya ugonjwa huo kusambaa kwa haraka katika eneo hilo lenye watu wengi lililo mpakani na nchi jirani ya Rwanda. Ugonjwa wa ebola uliibuka DRC mwezi Agosti mwaka uliopita na kusababisha zaidi ya vifo 1, 600 nchini humo.

 

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.