Star Tv

Moto uliozuka katika ghala la kuhifadhia pamba inayokadiliwa kuwa tani 120,000 limeteketeza pamba yote katika kijiji cha Shinyanga Mwenge kata ya Dakama wilayani Maswa mkoani Simiyu na kuwaachia kilio wakulima wa zao hilo waliouza pamba yao kwa mkopo.

Pamba hiyo iliyotekea inadaiwa ilikuwa na thamani ya shilingi milioni 144 iliyokuwa imenunuliwa na chama cha msingi(AMCOS) cha kijiji cha Shinyanga Mwenge kwa wakulima wa zao hilo.

Taarifa za awali zinadai kuwa chanzo cha moto huo ni kimetokana na mtoto mdogo aliyekuwa anachezea kiberiti aliwasha moto na kutupia pembeni mwa ghala hilo Lililokuwa wazi kwa chini Na hivyo kusababisha kushika moto.

Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Shinyanga Mwenge waliouza pamba yao katika chama cha msingi AMCOS hicho wameonyesha wasiwasi wao juu ya hatma ya malipo yao jinsi watakavyoweza kulipwa fedha zao kwa kuwa walikuwa wameuza kwa mkopo.

Mkuu wa wilaya ya Maswa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dkt Seif Shekilaghe amewaomba wakulima kuwa wavulivu na amewatoa hofu wakulima waliouza pamba watalipwa baada ya tathimini kufanyika.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.