Star Tv

Mamia kwa maelfu ya wakaazi wa Hong Kong wamefanya maandamano mjini humo jana kuupinga mpango wa serikali utakaoruhusu watuhumiwa kupelekwa China bara kukabiliwa na mashtaka.

Wakati maandamano hayo yalikuwa ya amani kwa kiasi kikubwa, mamia kadhaa ya waandamanaji walikabiliana na polisi nje ya bunge la mji huo jana jioni. Makundi madogo ya waandamanaji yaliahidi kupiga kambi nje ya bunge hadi Jumatano, wakati mswada huo unaolalamikiwa utakaposomwa kwa mara ya pili bungeni. Hata hivyo, walifurushwa na polisi wakati kibali chao cha kuandamana kilipomalizika muda wake usiku wa manane. Tukio hilo lilikuwa mojawapo ya maandamano makubwa kabisa katika historia ya Hong Kong, ambapo polisi walikadiria kuwa karibu waandamanaji 240,000 walishiriki. Lakini waandaaji wa maandamano hayo walisema karibu watu milioni moja walishiriki.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.