Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA) Juni nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao, na wanyama walao nyama na uwepo wa ukanda mrefu wenye wanyama wengi imepangwa kukabidhiwa kwa raisi Dkt John Magufuli.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Waziri Kigwangala,hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGT yanapofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugnzi TANAPA ,George Waitara amesema ushindi wa Hifadhi ya Serengeti kuwa Hifadhi Bora ni ushindi wa Watanzania wote. Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda amesema tuzo hiyo imepatikana baada ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushindanishwa na Hifadhi nyingine kubwa tano barani Afrika kwa watalii kupiga kura.